Picha:Afisa lishe jiji la Mwanza Emma Kilimali |
Na.Lucy
Sanka@cfjmedia
Wanawake Katika Jiji La Mwanza Wameaswa Kuwanyonyesha Watoto Wao Miezi Sita Ya Mwanzo
Pale Anaopojifungua Ili Mtoto Apate Kinga Mwilini Dhidi Ya Maradhi Mbalimbali
Na Kukua Katika Msingi Bora.
Hayo Yamesemwa Na Afisa Lishe Katika Jiji La Mwanza Bi
Emakilimali Ofisini Kwake Alipokuwa
Akizungumza Na Waandishi Wa Habari Ameeleza Kuwa Imebainika Kuwa Wamama Wengi
Siku Hizi Hawazingatii Masharti Ya Kunyonyesha Watoto Wao Badala Yale Wamekuwa
Wakinyonyesha Kwa Mazoea Bila Kuzingatia Utaalamu Wa Kiafya.
Aidha Bi Ema Kilimali Ameeleza Kuwa Mama Akimnyonyesha Mtoto Wake Kwa
Kuzingatia Utaalamu Wa Afya Mtoto Atakua
Kiakili Vizuri Lakini Pia Kuepusha Gharama Ya Kununua Maziwa Mbadala Na Kuepuka
Hata Uchafuzi Wa Mazingira Kutokutupa Makopo Ya Maziwa Ovyo.
Mbali Na Hayo Amewataka Wanawake Wanaonyonyesha Na Wanaotarajia
Kunyonyesha Siku Za Karibuni Wawanyonyeshe Watoto Wao Vizuri Waache
Kujidanganya Kuwa Akinyonyesha Mtoto Ata Haribu Shepu Yake Atakapo Nyonyesha.
Ikumbukwe Kuwa Kila Ifikapo Tarehe Moja Mwezi Wa Nane Hadi Tarehe Saba
Mwezi Wa Nane Ni Wiki Ya unyonyeshaji wa maziwa ya mama ambayo huadhimiswa Kila
Mwaka Ulimwenguni Kote.
0 Comments:
Post a Comment