SOMA KWA UFUPI HISTORIA YA MAMA MARIA NYERERE: ANATAMBUA UMUHIMU WA VIJANA

@CFJMEDIA Kuelekea miaka 19 ya Hayati Mwl.Nyerere.
Mama Maria Nyerere alizaliwa akijulikana kama "Maria Waningu Gabriel Magige" mnamo 31 Disemba 1930 alikuwa mke wa rais wa kwanza wa Tanzania Mwl Julius Kambarage Nyerere kuanzia 1964 hadi 1985. Kwa kawaida nchini Tanzania anajulikana kama 'Mama Maria' tu.
Mama Maria alikuwa mtoto wa saba kati ya tisa wa Mzee Gabriel Magige, wa Baraki, Tareme, kutoka kwa mkewe aliyejulikana kama Hannah Nyashiboha.
Maria alisoma katika shule ya "White Sisters' School" iliyokuwa Nyegina,Musoma Mara kisha akaenda shule ya Ukerewe, kisha akajiunga na chuo cha ualimu "Sumve Teacher Training College"; alihitimu kwa kupata cheti cha ualimu akaanza kufundisha katika Shule ya Msingi Nyegina iliyoko Musoma. Maria aliolewa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1953.Kwa sasa ni miongoni mwa wajumbe saba wa baraza la wazee wa "Alliance for Tanzania Youth Economic Empowerment" (Atyee), pamoja na rais wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Ali Hassan Mwinyi


pamoja na kuwa Maria Nyerere amekuwa na umri mkubwa takribani miaka 88 sasa lakini amekuwa akiamini sana katika vijana kwenye ujenzi wa Taifa Maneno haya aliyasema alipotembelewa na Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) TAIFA  tarehe 08/10/2018.Amewataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kuitumikia, kuipenda na kuilinda nchi yao ikiwemo kuwasemea, kuwatetea na kuwaunga mkono viongozi wazalendo wanaofanya kazi nzuri ya kuijenga nchi yetu ili kuwatia moyo. 

Mama Maria Nyerere ameipongeza kazi kubwa inayofanywa na Mhe Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli na amewaomba viongozi wote nchini, vijana na wananchi kumuunga mkono na kufanya juhudi kwenye maeneo yao ili kusaidia kuijenga Tanzania Mpya.

0 Comments:

Post a Comment