Mabula: Azidi kuchapa kazi


Picha: Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mh.Stanslaus Mabula akizungumza
Na Cornelius F. Shija @cfj media
Mbunge wa jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza Mh. Stanslaus Mabula amezungumza na wanahabari kutoka vyombo mbalimbali kutoka Mwanza na nje ya Mwanza, Katika kufikisha taarifa za miradi ya maendeleo ya jimbo Lake warsha hiyo imefanyika 20/JULY/2018 katika ukumbi wa New Mwanza Hotel Mwanza.

Mh.Mabula pia akijibu maswali yaliyoulizwa na wandishi wa habari amegusia juu ya swala la wafanya biashara wadogo wadogo maarufu kama machinga na kusema kuwa changamoto nyingi zinawakabiri wafanyabiashara hao na kusema kuwa wanandaa mikakati ya kuwaboreshea mazingira rafiki kibiashara
Ili kutambua idadi yao na aina ya biasahara wanayoifanya na kuwajengea uwezo wa ajira za kudumu

Pamoja na hayo mbunge huyo amesema kuwa halmashauri ya Nyamagana inajipanga kununua mashine ya kufyatulia tofali  ambapo mashine hiyo inauwezo wa kufyatua tofali 6000 kwa saa ili kuhakikisha wanapunguza changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa na kuwataka pia wadau na wawekezaji wadogo wadogo  wanajitokeza kusaidia ujenzi wa madarasa kuanzia ngazi ya msingi hadi ngazi ya renta, kisha halimashauri itamalizia upauaji madarasa hayo pamoja na madawati.

Picha : Muonekano wa baadhi ya wandishi wa habari kwenye warsha hiyo

























0 Comments:

Post a Comment