Miaka saba ya huduma ya kanisa la upendo

Picha:Pastor Prosper (Kushoto)

Na. cornelius F.Shija@Cfjmedia.

Kanisa la International pentecostal holness chuch lijulikanalo kama kanisa la Upendo jijini Mwanza limeadhimisha miaka 7 toka kuanzishwa kwa huduma hiyo ,kanisa hilo linapatika katika mtaa wa Mkuyuni sokoni chini ya Pastor Prosper William Magubo na mbeba maono wa kanisa hilo.

Sherehe hiyo imefanyika jumapili ya 29.July.2018 Katika kanisa hilo  na kuambatana na Ibada kubwa iliyongozwa na William Magubo ambapo amewataka watu wote waliohudhuria katika hafla hiyo kuto kufanya mchezo wawapo madhabahuni kwani kusifu kwa mzaha ni sawa na kujichumia dhambi na kuwakumbusha washirika kuwa kila mwanadamu ameumbwa ili atimize kusudi la Mungu.
Sherehe hiyo imerushwa mubashara kupitia kituo cha Radio cha Kwaneema fm radio(98.1)Mwanza na kupambwa na watangazaji wa Radio hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi mtendaji Mailande Mpemba pamoja na waimbaji wa nyimbo za injili kutoka sehemu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kumunga mkono mchungaji huyo kwa huduma yake ya kuutangaza ufalme wa mungu.
Picha:Wafanyakazi wa Kwaneemafm katika muonekano




















Picha:Watoto wakinogesha kwa kusoma Taarifa ya Habari





















0 Comments:

Post a Comment