Mwanza yazindua kampeni ya Furaha yangu


Na.Cornelius F.Shija@Cfjmedia
Mkuu wa mkoa wa Mwanza mh.John Mongella amekuwa mstari wa mbele kuwahimiza wananchi wa mkoa wa Mwanza kujitokeza kupima mambukizi ya virusi vya UKIMWI katika uzinduzi rasmi wa Kampeni ya Furaha yangu.

Mongella amesema hayo mbele ya wandishi wa habari ofisini kwake tarehe 19.July.2018 ikiwa ni mwendelezo wa uzinduzi wa kitaifa uliofanyika jijini Dooma 19. June.2018 Mgeni rasimi alikuwa ni waziri mkuu  Kasim Majaliwa lengo ikiwa ni kufikia 90 90 90  Tisini ya kwanza ni idadi ya kupima afya zao,Tisini ya pili ni watu kujua hali zao,na Tisini ya tatu baada ya watu kujua hali zao na kuanza kutumia dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi.

Katika mkoa wa Mwanza uzinduzi huu unafanyika katika viwanja vya Furahisha kuanzia saatatu asubuhi Jumamosi 21 .July.2018 .Dkt mkuu wa Mwanza Thomas Lutachunzibwa amesikitishwa na ongezeko la mambkizi ya virusi vya ukimwi kutoka asilimia 4 hadi kufikia asilimia 7.2 huku wanaume wakiongoza kutojitokeza kupima virusi vya ukimwi.


0 Comments:

Post a Comment