YALIYOJILI KATIKA 40 YA MUME WA MABULA

Picha:Mh.Angelina Mabula akiwa na ndugu Kirumba Makaburini

Na.Cornelius F. Shija@Cfj media.
Ikiwa zimepita siku kadhaa toka afariki Mume wa Mbunge wa jimbo la Ilemela Mh.Angelina Mabula mzee Julius Kakono Mabula aliyefariki tarehe 13.06.2018  Leo tarehe 31/08/2018 kumefanyika Ibada   nyumbani kwake Kirumba wilayani Ilemela mkoani Mwanza .Ibada hiyo imeongozwa na Paroko msaidizi wa Parokia ya Kirumba Riziki Ngoi na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serkali pamoja na  watumishi wa mungu  mbalimbali pamoja na mashekhe.
Katika Ibada hiyo Paroko Riziki amewaomba wanafamilia kumuomba Mungu awape uvumilivu kwa kwa kuwa kila mmoja ataelekea katika makao hayo ya milele

Baada ya Ibaada ya nyumbani
waombolezaji wote waliekea katika makaburi ya kirumba kanisani
wakiongozwa na waziri wa nyumba na maendeleo ya makazi Bi Angelina mabula pamoja na wanafamilia kwa ujumla.



Picha:Kwaniaba ya familia Mzee Peter Madaha Segeja amewashukru watu wote waliofika nyumbani hapo kwa ajili ya maombolezo ya siku 40 ya Marehemu.Julius Kakono Mabula.



0 Comments:

Post a Comment