Picha:Mwenyekiti wa Chemba ya wafanya biashara Mkoani Mwanza Elbariki M. Mrari
Na.Cornelius F. Shija@Cfj media Maonesho ya biashara ya Afrika mashariki yanayoandaliwa na Chemba ya wafanya Biashara mkoa wa Mwanza(TCCIA) yameanza leo tarehe 31.Agoust,2018 chini ya Mwenyekiti wa Chemba hiyo Elbariki M. Mrari, Ambapo amewataka watu wote kuchangamkia fursa ya maonesho hayo ambayo awamu hii yamejumuisha nchi washiki wa East Africa Community isipokuwa nchi ya Burundi pekee.
Maonesho haya yatazinduliwa rasmi tarehe 04,Septemba,2018 katika eneo la nje la Rockcity Mall na mgeni rasmi anayetarajiwa katika uzinduzi huu ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Charle Mwijage na yatadumu kwa takribani siku 10 toka uzinduzi huo.
Pamoja na hayo wananchi wanakaribishwa kwa ajili ya kuchukua Mabanda kwa ajili ya maonesho hayo kwani maeneo yameongozeka ya kufanyia maonesho hayo kutoka sq mita 15 kwa bei ya laki tisa mwaka jana hadi ukubwa wa sq mita 23 kwa bei ileile kwa mwaka huu. |
0 Comments:
Post a Comment