YUHOMA YAGAWA VIFAA VYA MICHEZO KWA WANAFUNZI MWANZA

.

Picha:Mkurugenzi mkazi (YUHOMA)kanda ya ziwa Yusuph Yahaya
Na.Cornelius F.Shija@Cfj media
Taasisi ya ambayo inajishughulisha na kuwatafutia wanafunzi vyuo vikuu nje ya nchi ya Yuhoma Education Limited(YEL) yenye makao makuu Jijini Mwanza katika jengo la Nyanza Gorofa ya pili katika chumba No.204 Barabara ya Kenyatta, I,etoa elimu kwa wanafunzi pamoja na vifaa vya michezo kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Butimba kutwa na shule ya Sekondari Kangae kwa lengo la kuunga juhudi za Serkali ya awamu ya tano kwenye michezo na kutatua changamoto za wanafunzi hao

Akigawa vifaa hivyo mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bw. Yusufu Yahaya katika maonesho ya awamu ya kumi na tatu ya East Afrika tarehe 01,Septemba,2018  ambayo yanafanyika katika eneo la Rock city mall Mwanza, Amewataka wanafunzi hao kutoka shule hizo kuwa na Juhudi katika masomo yao ili kufikia ndoto zao na  kuweza kuwasaidia wote wataokuwa na sifa za kuenda kusoma vyuo vikuu nje ya Nchi na kuwataka pia kuwa mabalozi wakuu wa taasisi hiyo kupitia michezo .
 Taasisi hiyo imewapatia wanafunzi wa Shule ya Kangae sekondari pamoja na Butimba Sekondari Jezi pamoja na mipira ya mchezo wa miguu.

Picha: Mwanafunzi Salum Hamis kidato cha pili kutoka Shule ya sekondari Kangae aliyeshinda zawadi ya kiasi cha Pesa shilingi Elfu kumi kutoka kwa Mkurugenzi baada ya kupiga Danadana mia moja




TAZAMA VIDEO HAPA CHINI NIMEKUWEKEA

0 Comments:

Post a Comment