WATUMISHI WA MUNGU WAKUTANA NA KWANEEMA FM

Picha:Muonekano wa pamoja wa Maaskofu,Wachungaji pamoja na watangazaji wa Kwaneema fm

Na.Cornelius F.Shija@Cfj media
Watumishi wa Mungu ikiwemo Maaskofu pamoja na Wachungaji wa makanisa mbalimbali kutoka Jijini Mwanza wamekutana na Uongozi wa Kwaneema fm(98.1 Mwanza) katika kujadili namna ya kushirikiana katika kujenga Ufalme wa Mungu,Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 30,Agoust,2018 katika ukumbi wa Waste Land Mwanza.

Mkutano huo umendeshwa na Mkurugenzi msimamizi wa radio hiyo Mailande Mpemba, ambapo amewaomba watumishi hao kusaidia katika ununuzi wa Mnara kwa kuchangia pesa na kuwashirikisha washirika wa makanisa yao ili kuondokana na usumbufu na gharama kubwa ya kupanga katika minara mingine

Pamoja na hayo Mkurugenzi huyo amezungumzia juu ya Sherehe kubwa ya kuadhimisha miaka minane(8) Toka kuanzishwa kwa Radio hiyo itakayo fanyika tarehe 27,Oct,Mwaka huu .
Picha: Muonekano katika picha ni Uongozi wa Kwaneema fm

0 Comments:

Post a Comment