THE DESK & CHAIR FOUNDATION: TUKIACHA KUBAGUANA WATANZANIA TUNAWEZA

Na.Cornelius F.Shija@Cfjmedia
Mwenyekiti wa Taasisi ya "THE DESK & CHAIR FOUNDATION" Sibtain P. L.Meghjee yenye makao makuu yake katika jijini Mwanza  amesema kuwa watanzania wanatakiwa kuacha tabia ya kubaguana kwa vigezo vya Dini,Siasa,Rangi kwani kufanya hivyo kunasababisha utengano na kujiona watanzania hatuwezi hata katika mambo madogo madogo kama vile kusaidia ujenzi wa vyoo mashuleni,madawati,n pamoja na huduma zq Afya hususani vijijini.

Tasisis hii imekuwa ikijihusisha na mambo ya kijamii nchini kama kuchimba visima vya kudumu, kuwapatia viungo vya bandia walemavu wa miguu na mikono,kuwapatia mitaji wafanya Biashara wadogo wadogo,pamoja na kushiriki katika uchangiaji wa damu salama nchini, 
Sibtain amevishukuru vyombo vya habari mbalimbali na serkali kwa kuitangaza vyema taasisi hiyo katika jamii hali ambayo imepelekea idadi kubwa ya watu ambao wanafika kwa ajili ya mahitaji ya misaada mbalimbali hali ambayo imepelekea uhitaji mkubwa wa wadhamini ambao wanaweza kusaidiana nao kuisaidia jamii ya watanzania.

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI KWA KINA ZAIDI:

0 Comments:

Post a Comment