MWIJAGE:DUNIA HII NI YAKUSHUGHULIKIANA, KUCOPY NA KUPASTE ISIKUPE SHIDA




Na.Cornelius F.Shija@Cfjmedia
Waziri wa Viwanda  Biashara na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage amewapa neno zito wafanya Biasahara na wajasiriamali nchini juu ya kufanya ujasiriamali wenye tija na kujifunza kupitia maonesho ya bidhaa na kutafuta wateja  na kungalia wengine wanafanya nini ili kujifunza.

Mwijage ameyasema hayo tarehe 04,septemba,2018 katika uzinduzi wa maonesho ya Biashara ya Afrika mashariki katika viwanja vya Rockcity mall Jijini Mwanza yanayojumuisha nchi wanachama wa (East Africa Community) ambayo yanahitimishwa rasimi tarehe 09,sept,2018.

"Wawekezaji, wajasiliamali wetu lazima tufanye ujasiriamali wenye tija,Tunakwenda kwenye maonesho kwanini? kutafuta wateja kupitia kwenye bidhaa zetu lakini jambo jingine nikuangalia wenzetu wanafanya nini ili kutoka kwao twende kujifunza, yaani ile copy and paste "Mtu akikuambia copy and paste kama inatija wewe inakusumbua nini?" TAZAMA VIDEO HAPA CHINI

0 Comments:

Post a Comment