MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA(TCRA) YAFANYA MKUTANO NA WATEJA WAO JIJINI MWANZA KUHUSU MKATABA NA MAPAMBANO YA RUSHWA

Na.Cornelius F.Shija@Cfj media
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania(TCRA) Wamefanya mkutano kuhusu Mkataba kwa wateja wa Tcra na Mapambana dhidi ya Rushwa kwa viongozi wa juu wa Makampuni yenye Leseni za Mawasiliano Kanda ya ziwa,Mkutano huo umefanyika katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza leo tarehe 24.septemba.2018. Akizungumzia juu ya Rasimu ya mkataba huo ambayo ilizinduliwa rasmi tarehe 16,July,2018 Katika ofis za Makao makuu ya Tcra Dar es salamu,

Akizungumza mbele ya Wandishi wa habari na wadau wa huduma za mamlaka hiyo Lawi Odiero ambae ni mhandisi wa (TCRA) Kanda ya ziwa amesema kuwa mkataba huu ni wakwanza kuundwa tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo, Nakuongeza kuwa wataendelea kukutana na wadau mbalimbali wa huduma za mawasiliano ili kutoa maoni na kukosoa kabla ya kuchapishwa kwa rasimu ya mkataba huo.”Mktaba huu utakuwa chachu ya kuboresha utoaji huduma ili kuwaridhisha wateja wetu na hivyo kuchangia uboreshaji wa huduma za Umma tunaomba ushirikiano wenu katika taratibu za kukamilisha na kutekeleza huu mkataba”  

Katika mkutano huo Taasisi ya kudhibiti na kupambana na rushwa TAKUKURU wameshiriki kutoa elimu kwa wadau juu ya kuwa kumbusha kutojihusisha na vitendo vya rushwa kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria,Pia wandishi wa habari walipata nafasi ya kuuliza maswali kuhusu huduma za Umma kutoka TAKUKURU na TCRA. TAZAMA HAPA CHINI MAJIBU:

0 Comments:

Post a Comment