TACAIDS NA UTAFITI WA VVU

Picha:Mkurugenzi wa uraghbishi(TACAIDS) Jumanne Issando
Na.Cornelius f.Shija@CFJMEDIA.
Tume ya kupambana na kuzuia mambukizi ya virusi vya Ukimwi Tanzania bara (TACAIDS) wameendesha Mkutano na wanahabari kutoka radio mbalimbali za kijamii(Community radios) Lengo ni kutoa habari ya juu ya utafiti wa kitaifa wa viashiria na matokeo ya  UKIMWI kwa  2016/2017(THIS)Tanzania HIV Investigation search

Akizungumza mgeni rasimi Mr.Jumanne Issando Mkurugenzi  uraghbishi  kutoka Tacaids amegusia juu ya kampeini ya  FURAHA YANGU iliyozinduliwa 19 June 2018 na Waziri mkuu  Kasimu Majaliwa Jijini Dodoma na kuwakumbusha wanaume kuitikia wito wa kupima afya na kutambua hali zao kwani ni wanaume 44 pekee katika asilimia mia ndiyo wanatambua hali zao

Kutokana na takwimu zilizofanywa na ofisi ya tafiti ya taifa NBS  Huu ni utafiti wa awamu ya nne ambao pia utatumika kwa miaka mine ili kufikia 90, 90, 90, ambapo tisini ya kwanza ni wanaoishi na vvu na kutoa taarifa kuwa wanamambukizi ya vvu,Tisini ya pili ni walio kwenye matibabu na waliotoa taarifa kuwa wanatumia dawa za kufubaza makali ya vvu (ARV,ARV) Na Tisini ya tatu ni asilimia ya kufubazwa kwa vvu.
Aidha Jumanne Issando  Taarifa za utafiti wa 2016/2017 zinaonyesha kuwa kiwango cha mambukizi ya virusi vya ukimwi  ni asilimia 4.7 kitaifa ambapo wanawake ni asilimia 5.0 na wanaume 6.5 ya maambuzi yaote, hata hivyo watu wanasisitzwa kujitokeza kupma mapema ilikupunguza idadi ya mambukizi mapya kwani  kati ya watu waliopima ukimwi asilimia 52 waanajua hali zao na asilimia 42 hawajui hali zao.
Picha:Wandishi wa habari kutoka Radio za kijamii kwenye mkutano wa (TACAIDS)










0 Comments:

Post a Comment