Na.Cornelius F. shija @CFJMEDIA TZ.
Mkoa wa mwanza leo19.june umeungana na mataifa mengine
duniani katika maadhimisho ya ugonjwa wa
siko seli pamoja na kutoa semina kwa wazazi ili kutambua maana ya ugonjwa wa seli mundu namna ya kupata vipimo pamoja na matibabu
yake.
akizungumza katika maadhimisho hayo mganga bingwa wa watoto dr.emmanuela ambrous amesema
kuwa ugonjwa wa seli munu umekuwa tishio kubwa kwa watoto na kuwataka wazazi
pamoja na jamii kujenga mazoea ya kupima ugonjwa huo
akizungumza mmoja
wa wazazi bi. juliana kutokea
nyegezi amesema kuwa hakutambua mara
moja juu ya ugonjwa wa mwanae
unaomsumbua kwa kuwa dalili zilifanana na malaria pia amewaomba wababa
wasiwalaumu wake zao juu ya ugonjwa huo kuwa wao ndio chanzo.
nae elikana nyanda pamoja na
wadau mbalimbali wamezungumzia juu ya ugonjwa huu pia elikana kama kijana amejikita
kuzungumzia uzoefu wa kuishi na ugonjwa siko seli katika maeneo ya kazi
,jamii na shuleni kwa miaka 32,
aidha pia dr. emmanuela ametoa rai kwa jamii kuacha
dhana hiyo potofu iliyopo ya kuhani siko
sekli kwa mtoto inasababishwa na mama pekee, bali wazazi wote mmoja akiwa na
vimelea na mwingine akiwa na siko seli
TAZAMA VIDEO:MAMA MWENYE MTOTO WA SIKO SELI
0 Comments:
Post a Comment