TAHARUKI YA MOTO KUTEKETEZA SOKO LA MLANGO MMOJA JIJINI MWANZA


Na.Cornelius F.Shija@Cfjmedia
Wafanya biashara wa bidhaa mbalimbali za nguo,viatu,washona nguo pamoja na Mama lishe wanaofanya biashara katika soko la Mlango mmoja  maarufu kama (Lango lango) Nyamagana jijini Mwanza wamelazimika kustisha shughuli zao kufuatia moto mkubwa uliozuka na kuteketeza baadhi ya vibanda na Maduka yao usiku wa kuamkia leo 28.septemba 2018

Akielezea Mwenyekiti wa mtaa wa Uhuru Bi.Chuki Husein eneo lilipo soko la Mlango mmoja amesema kuwa" nilipigiwa simu na walinzi wa soko hilo majira ya saa tisa na nusu usiku na kuambiwa kuwa soko linaungua kuja kuangalia upande wa kushoto ambapo mama ntilie hufanya biashara ndipo moto umeanzia" na amewataka wafanyabiashara hao kuwa na subira wakati taratibu zikiendelea.

Kwa upane wake mkuu wa wilaya ya Nyamagana Dr. philis Nyimbi Meshaki amesema kuwa chanzo cha moto huo bado hakijajulikana kutokana na kuwa bado jeshi la polis linaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo na kuwataka wafanya biashara hao kuwa na uvumilivu na utulivu na  kuendelea kutoa ushirikiano kwa baadhi yao na jeshi la polis

Naye kamanda wa jeshi la [polisi mkoa wa Mwanza Jonathan Shana amewaonya wale wote wanaotaka kutumia mwanya huo kwa ajili ya kuiba watawakamata na kuwaunguza kwa moto huo na kuwa majivu"Kama unavyoona mpaka sasa hivi hakuna hata kitu kimoja kitaibiwa na niawaonye wale wote wanaotumia mwanya huu kuiba waache huu moto unao waka hapa tutawatekeketeza watabaki jivu kabisa hakuna atakae baki"Amesema kamanda Shana.
Tazama picha zaidi za tukio......Endelea kukaa karibu na Cfjmedia kwa Taarifa zaidi.





0 Comments:

Post a Comment