SHULE INAYOWAFUNZA WAVULANA KURIPOTI DHULUMA DHIDI YA WANAWAKE NA KUWALINDA NCHINI RWANDA


Tokeo la picha la picha za wanafunzi
Chanzo:BBC Swahili.
Katika kijiji kilicho nje ya mji mkuu wa Rwanda Kigali, kundi la wavulana wanatumia muda wao wa jioni kujifunza jinsi ya kuzuia dhuluma za kijinsia na kuwepo usawa katika kile kinachotajwa kama #MeToo era.

Huku wasichana wakijifunza kuhusu uwekezaji na njia za kijitegemea kifedha pamoja na afya ya uzazi na jinsi ya kudhibiti familia zao miaka inayokuja, wavulana hufunzwa jinsi ya kuripoti dhuluma na pia kuwaheshimu wanawake katika maisha yao.Mafunzo haya hufanyika baada ya masomo ya kawaida.
Kila siku jioni wavulana na wasichana hugawanyika kujifunza njia tofauti za kuboresha maisha ya wanawake kote nchini Rwanda.Kwa wavulana ni wakati wa kuambiwa kuwa ni jukumu la wanaume kumaliza ghasia. Ni jukumu la wavulana na wanaume kuripoti dhuluma.
"Ikiwa tutaona ghasia kama hizo, tunaziripoti na kuhakikisha kuwa wale watu ambao wamezitekeleza wameshtakiwa, Rini Mutijima mwenye miaka 18 katika shule hiyo aliiambia BBC.
Wakati ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 hadi wanawake 500,000 walibakwa wakati wa kipindi cha siku 100 cha umwagaji damu, ambapo makundi ya wahutumu yaliwaua watusi 800,000 na wahutu wenye msimamo wa wastani.Hata hivyo taifa hilo dogo la mashariki mwa Afrika limekiuka vizuizi na kuwa kielelezo cha usawa ya jinsia barani Afrika.
Rwanda ina wakawake wengi zaidi kwenye serikali duniani wakati zaidi ya asilimia 60 ya wabunge nchini Rwanda wakiwa ni wanawake.
Nchi hiyo inajivunia katika uwakilishi wa wanawake serikalini licha ya ubaguzi ya jinsia kuwa mkubwa kati ya watu wanaoishi vijijini.
Takriban asilimia 27 ya wanawake nchini Uingereza na asilimia 25 ya wanawake nchini Marekani hukumbwa na dhuluma kutoka kwa wanaume katika maisha yao, huku Umoja wa Mataifa ukikadiria asilimia hiyo kuwa 34 nchini Rwanda.Kwenye shule iliyo wilaya ya Ruhango, suala tofauti huzungumziwa kila siku.
Siku moja wavulana wanaweza kujifunza kuhusu hedhi na siku itakayofuata jinsi ya kuzuia kuwadhulumu wanawake kifedha.
Kisha mara moja kwa wiki wavulana hushiriki katika mjadala kuhusu vile wanaweza kumaliza ghasia za kijinsia.
Shule hizo zilizo kote Rwanda zinewafunza zaidi ya wasichana 47,000 na wavulana 19,000 tangu mwaka 2015.
"Tunasoma Historia, anasema Patience Manzi, mvulana wa miaka 16." tunasoma vitu hivi kuelewa kuhusu siku zilizopita na hii hutusadia kuzuia wengine kuwapiga wake zao."
Shoffy Manishimure, mvulana mwingine wa miaka 16 aliongeza: "Kitu kizuri zaidi nimejifunza ni kuhusu kumlinda dada yangu.
"Ni jukumu langu kama mvulana kumlinda dada yangu."
Programu zingine zinazowahusisha wanaume tayari zimeonekana kufanikiwa katika kupunguza dhuluma dhidi ya wanawake Rwanda.











0 Comments:

Post a Comment