NDEGE MPYA AINA YA BOEING737 YAANGUKA JAKARTA INDONESIA


Ndege ya kuwabeba abiria ya shirika la Lion Air aina ya Boeing 737 imeanguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege mjini Jakarta, maafisa wa Indonesia wamesema.
Ndege hiyo safari nambari JT-610 iliyokuwa imewabeba abiria 188 ilikuwa safarini kutoka mji huo mkuu wa Indonesia kwenda Pangkal Pinang, jiji linalopatikana katika visiwa vya Bangka Belitung.
Iitoweka kutoka kwenye mitambo ya rada saa kadha baada ya kupaa, ilipokuwa inavuka bahari.Katika kikao na wanahabari, maafisa wamesema ndege hiyo, ambayo ni ndege mpya aina ya Boeing 737 MAX 8, ilikuwa imewabeba abiria 178 watu wazima, watoto watatu, marubani wawili na wahudumu watano wa ndege.
Yusuf Latif, msemaji wa shirika la huduma za uokoaji na kuwatafuta manusura amewaambia wanahabari: "Imethibitishwa kwamba ndege hiyo imeanguka."
Afisa wa shirika hilo la ndege amesema bado hawajui chanzo cha kuanguka kwa ndege hiyo.
Afisa mkuu mtendaji Edward Sirait ameambia shirika la habari la Reuters: "Hatuwezi kusema chochote kwa sasa. Tunajaribu kutafuta maelezo na data zaidi."Vyombo vya habari Indonesia vimemnukuu afisa wa bandarini Tanjung Priok akisema kwamba maafisa wa boti la kusindikiza meli wameripoti kwamba wameviona vifusi vya ndege hiyo kwenye mai.
Suyadi, ambaye hutumia jina moja pekee kama raia wengi wa Indonesia, amesema vyombo vingine vya baharini vimefunga safari kuelekea eneo hilo.Indonesia, taifa kubwa la mkusanyiko wa visiwa, hutegemea sana uchukuzi wa ndege, lakini ina historia ya ajali nyingi za ndege.Mwaka 2013, ndege ya Lion Air safari nambari 904 ilianguka baharini Bali ikijaribu kutua uwanja wa ndege wa Ngurah Rai.
Abiria wote 108 waliokuwa kwenye ndege hiyo walinusurika.
Mwaka 2004, ndege nyingine ya Lion Air safari nambari 538 kutoka Jakarta ilianguka na kuvunjika vipande vipande ilipokuwa inatua mjini Solo na kuwaua watu 25.

SHUHUDIA HARUSI YA MTANGAZAJI WA KWANEEMA FM MWANZO MWISHO;



Na.Cornelius F.Shija@Cfjmedia
Mtangazaji wa Kwanema fm Radio Godwin Deus maarufu kama "Brother G" hatimaye ameuaga ujana baada ya kuingia rasmi katika ndoa na Mwana dada ambaye ni mtangazaji kutoka Tarime( Mara) Catherine Mniko.

Ndoa hiyo imefungwa tarehe 14.10.2018 katika kanisa la E.A.G.T. HEBRON NYAKABUNGO na baadae sherehe ikafanyika katika ukumbi wa BELMONT FAIRMOUNT HOTEL(JB).
TAZAMA  VIDEO ILIVYOKUWA  HAPA CHINI:

SOMA KWA UFUPI HISTORIA YA MAMA MARIA NYERERE: ANATAMBUA UMUHIMU WA VIJANA

@CFJMEDIA Kuelekea miaka 19 ya Hayati Mwl.Nyerere.
Mama Maria Nyerere alizaliwa akijulikana kama "Maria Waningu Gabriel Magige" mnamo 31 Disemba 1930 alikuwa mke wa rais wa kwanza wa Tanzania Mwl Julius Kambarage Nyerere kuanzia 1964 hadi 1985. Kwa kawaida nchini Tanzania anajulikana kama 'Mama Maria' tu.
Mama Maria alikuwa mtoto wa saba kati ya tisa wa Mzee Gabriel Magige, wa Baraki, Tareme, kutoka kwa mkewe aliyejulikana kama Hannah Nyashiboha.
Maria alisoma katika shule ya "White Sisters' School" iliyokuwa Nyegina,Musoma Mara kisha akaenda shule ya Ukerewe, kisha akajiunga na chuo cha ualimu "Sumve Teacher Training College"; alihitimu kwa kupata cheti cha ualimu akaanza kufundisha katika Shule ya Msingi Nyegina iliyoko Musoma. Maria aliolewa na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1953.Kwa sasa ni miongoni mwa wajumbe saba wa baraza la wazee wa "Alliance for Tanzania Youth Economic Empowerment" (Atyee), pamoja na rais wa zamani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Ali Hassan Mwinyi


pamoja na kuwa Maria Nyerere amekuwa na umri mkubwa takribani miaka 88 sasa lakini amekuwa akiamini sana katika vijana kwenye ujenzi wa Taifa Maneno haya aliyasema alipotembelewa na Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) TAIFA  tarehe 08/10/2018.Amewataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kuitumikia, kuipenda na kuilinda nchi yao ikiwemo kuwasemea, kuwatetea na kuwaunga mkono viongozi wazalendo wanaofanya kazi nzuri ya kuijenga nchi yetu ili kuwatia moyo. 

Mama Maria Nyerere ameipongeza kazi kubwa inayofanywa na Mhe Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli na amewaomba viongozi wote nchini, vijana na wananchi kumuunga mkono na kufanya juhudi kwenye maeneo yao ili kusaidia kuijenga Tanzania Mpya.

UKITAKA KUANZISHA BIASHARA FANYA YAFUATAYO

Na.Cornelius F.Shija@Cfjmedia.
Leo 02,October,2018 nakukutanisha na Mwalimu na Mjasiriamali Mailande A. Mpemba kutokea taasisi ya Angaza na Maendeleo, akizungumzia namna ya kuanzisha biashara yako ambayo umekuwa ukiitamani.

Mailande amesema akiwa katika kipindi cha Angaza na maendeleo kupitia Kwaneema fm(98.1) Mwanza leo asubuhi jumanne
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI :